
Lowassa awaonya wanaomfuatafuata; awaita ‘wazushi’
Mbunge wa Monduli Bw. Edward Lowassa amesema kuwa kauli mbalimbali zinazotolewa na wanasiasa kupitia vyombo vya habari zikimhusisha yeye na mpango wa kuihujumu serikali ya Rais Kikwete au Chama cha Mapinduzi ni za kinjozi, hazina ukweli, na haelewi lengo lake hasa ni nini. Akizungumza na waandishi wa habari jimboni kwake Monduli leo Bw. Lowassa amesema kuwa “watu wanaopenyeza taarifa hizi katika vyombo vya habari wanafanya hivyo kwa malengo ya kufikiria ya kujisafishia njia za kisiasa”Bw. Lowassa alikuwa na kauli rasmi iliyoandikwa kwenye kurasa tano aliyokuwa ameianda na kuisoma mbele ya waandishi wa habari. Alikanusha vikali madai kuwa ana mpango wowote wa kumhujumu Rais Kikwete au Chama cha Mapinduzi ambacho yeye ni mbunge wake. “Ni jambo lisiloingia akilini kunihuisha na kile kinachoitwa mikakati ya kumhujumu rais au chama ambacho mimi ni kada wake wa muda mrefu, mbunge anayetokana na chama hicho hicho na mtu ninayeiongoza Kamati nyeti ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na zaidi ya yote kiongozi wa ngazi mbalimbali za kisiasa na kiserikali nilizowahi kushikilia” alisema Bw. Lowassa kwa msititizo.
Aliendelea na kusema kuwa licha ya kwamba hajawahi kufikiria kuibua “mabaya ya Rais Kikwete” hayo yanayoiwa “mabaya” yeye hayajui. “Mbali ya ya ukweli kwamba huo ni uongo wa wazi, silka yangu kama mwanasiasa na mtu mwenye dhamana kubwa kwa watu wa Monduli kwa taifa languhaiwezi kamwe kunituma nianz
No comments:
Post a Comment