Thursday, January 5, 2012

Jaribio la kuiba dhahabu katika mgodi wa Geita (GGM) lazimwa

Jaribio la kutaka kuiba kiasi kikubwa sana cha dhahabu ktk mgodi wa Geita mchana huu mida ya 11:30hrs na watu wenye silaha nzito za kivitaa limezimwa na walinzi wa mgodi (snipers & quick respond unit force wakishilikiana na makomandoo walinzi wa ndege inayosafirisha dhahabu) mpaka mida hii imethibitika watu 2 wamepoteza maisha.

Jaribio hilo limefanyika Ktk airport ya mgodini wakati dhahabu hiyo ikipakiwa ktk ka ndege special tayari kwa kusafirishwa kwenda South Africa, hadi mida hii wana Geita bado tunasikia milio ya risasi zikilindima maporini na ving’ora vya ambulance za mgodini zikiwabeba majeruhi wengi wao ni walinzi wa wa mgodi, polisi walitarifiwa mapema kabisa lakini bado wanajipanga namna ya kufika eneo la tukio!


Tutazidi kuajuza kadri nitavyo pata habari zaidi.

UPDATE:
Polisi wamefika eneo la tukio na kwa sasa wanawakamata wakata mbao, wachungaji na wachoma mkaa wakiwatuhumu kwa ‘ujambazi’ wakati wapiga deal halisi wameisha sepa , walinzi 8 wa mgodini ( wa kitanzania) wameahidiwa 10,000 USD kila mmoja kwa kuweza kulinda mali ya ’ mwekezaji’, huku mlinzi mzungu akisafilishwa kurudi RZA kwa matibabu ( huyu jamaa amepigwa kama risasi 3 mkononi na mguuni, na huyu ndio aliyeuwa jambazi baada ya kukabiliana naye uso kwa uso).

Polisi wamekabidhiwa sub machine gun 3, mabomu ya mkono 9 ( moja lilirushwa lakini halikulipuka vizuri) magazine zaidi ya 5 zikiwa na risasi zaidi 100, bullet proof vest 2.

Polisi wanasomeshwa wakubali kuwa wao ndio waliopambana na ku uwa majambazi ili hawa jamaa wanakwepa lawama za mauaji kimtindo, Mwili wa jambazi (kipande cha jibaba lenye asili ya kisomali inaaminiki ndiye alikuwa kiongozi wa uvamizi) umepelekwa mortuary, nikifanikiwa nita upload picha ya maiti yake.

Hali ya hewa imetulia kidogo na shuguli za kumtumikia kaburu zimeanza mnamo 1330hrs, kwa ujumla kulikuwa na vitofali 34 vya dhahabu ( kila kitofali kina 24KG) vilivyo pona pona kutembea ( ila nawalaumu hawa ma intruders kwa uchoyo wao!)

No comments:

Post a Comment