Friday, October 21, 2011

HIZI HABARI NIMENUKUU KUTOKA KATIKA MACHIMBO YA NEWS SIO MIMI ILA PATENI TU UKWELI JUU YA MAMBO YA LIBYA!

""Jana nilishindwa kutoa tamko langu kufuatia kifo cha Jemedali Colonel Gadafi kutokana sababu za Kiusalama... sasa basi kabla cjaongea lolote ikumbukwe kwamba hakuna watu wanaoielewa Libya tofauti na Walibya wenyewe, Kwamujibu wa CNN, BBC, Euro news na vituo vingine vingine vya Magharibi walitujaza Propaganda kwamba walibya wanataka demokrasia na hawamtaki Shetani ibilisi Gadafi,.. Hapo mwanzo niliamini ni kweli walibya wamechoshwa na utawala wa Gaddafi na Lindi la umaskini waliokuwa nao ila kujiridhisha zaidi nikaamua kufanya utafiti ili kuwa 100% sure kwamba kweli Walibya ndo wanachotaka.. Niliyoyakuta ndugu zangu hakuna hata mmoja nimewahi kusikia yakitangazwa na CNN wala BBC... Hebu tuone Libya Chini ya Utawala wa Gaddafi Ilikuaje; (Viwango Hivi ni Exchange rate ya sasa) 1. Pato la Mwananchi wa Libya wa Kawaida ni Sh. 24 Million 2. Kama Hauna Ajira unalipwa sh. 1.2 Million 3. Mshahara wa nurse Daraja la Chini sh. 1.7 Million 4. Kwa kila mtoto anaezaliwa analipwa 12 Million 5. Ukioa we na mkeo mnapewa Million 109 kununulia Makazi kwa ajili ya Familia Yako 6. Elimu ni Bure 7. Kutibiwa Hospitali yoyote ni Bure 8. Kusoma Nje ya Libya unalipiwa Kila kitu na Serikali. 9. Umeme Bure. 10. Marufuku unywaji Pombe marufuku 11. 85% ya watu wa Libya walikuwa wamesoma toka 25% alipochukua madaraka. 12. Hakuna Kodi Ya aina yoyote. 13. Ukithibitika umefanya Ufisadi unanyogwa. 14. Ukiuza Bidhaa zilizoexpiry au bandia Unanyogwa, kufungiwa leseni au faini kubwa au vyote kwa pamoja. 15. Lita ya Mafuta Haiuzwi zaidi ya sh. 160 16. Hakuna Riba kwenye mkopo wowote. 17. Ukinunua Gari karibia 50% unalipiwa na Serikali na kwa wanajeshi ni 65%. Jamani Yako Mengi tu... Sasa swali Langu ni Hili Walibya wanataka Demokrasia ili wawe kama Tanzania? maana cc tuna demokrasia sana tu na matokeo yake ndo haya.. Walibya waliwahi kuthubutu kusema wanatamani Maisha ya Nchi zingine sasa swali Je wanatamani mgao wa umeme? wanatamani Ufisadi? Siwasemei moyo ila ninachofahamu Libya ilikuwa pepo kama utaishi bila kuichokoza serikali.... Sasa Basi cc wenye demokrasia, haki za binadamu pamoja na utawala bora tunaishi maisha haya... Nawahakikishia Hawa Vibaraka wa Ulaya na Marekani wanaojiita National Transition Council (NTC) kamwe hawawezi kuipeleka Libya mahala popote zaidi ya Kuwapelekea Mafuta mabwana Zao wazungu.., Nawakaribisha Walibya kwenye Kodi zisizo na kichwa wala miguu,.. karibuni kwenye Lita ya mafuta 2000 kwa sababu hata Nigeria wanachimba mafuta ila ni Gharama Kubwa kama cc.... Ningesema mengi ila Waswahili wanasema MSIBA CHA KUJITAKIA HAUNA KILIO.. Tuombe Uhai Tunaonana Baada Ya miaka 5 halafu tuone Libya itakuaje.... Wapi IRAQ baada ya SADAM.., WAp AFGHANISTAN.. Iko wap KOSOVO... Kokote Nchi za Magharibi wanapoingilia huwa hapatulii kamwe.., R.I.P Colonel"'