HIZI HABARI NIMENUKUU KUTOKA KATIKA MACHIMBO YA NEWS SIO MIMI ILA PATENI TU UKWELI JUU YA MAMBO YA LIBYA!
""Jana
nilishindwa kutoa tamko langu kufuatia kifo cha Jemedali Colonel Gadafi
kutokana sababu za Kiusalama... sasa basi kabla cjaongea lolote
ikumbukwe kwamba hakuna watu wanaoielewa Libya tofauti na Walibya
wenyewe, Kwamujibu wa CNN, BBC, Euro news na vituo vingine vingine vya
Magharibi walitujaza Propaganda kwamba walibya wanataka demokrasia na
hawamtaki Shetani ibilisi Gadafi,.. Hapo mwanzo niliamini ni kweli
walibya wamechoshwa na utawala wa Gaddafi na Lindi la umaskini waliokuwa
nao ila kujiridhisha zaidi nikaamua kufanya utafiti ili kuwa 100% sure
kwamba kweli Walibya ndo wanachotaka.. Niliyoyakuta ndugu zangu hakuna
hata mmoja nimewahi kusikia yakitangazwa na CNN wala BBC... Hebu tuone
Libya Chini ya Utawala wa Gaddafi Ilikuaje; (Viwango Hivi ni Exchange
rate ya sasa) 1. Pato la Mwananchi wa Libya wa Kawaida ni Sh. 24 Million
2. Kama Hauna Ajira unalipwa sh. 1.2 Million 3. Mshahara wa nurse
Daraja la Chini sh. 1.7 Million 4. Kwa kila mtoto anaezaliwa analipwa 12
Million 5. Ukioa we na mkeo mnapewa Million 109 kununulia Makazi kwa
ajili ya Familia Yako 6. Elimu ni Bure 7. Kutibiwa Hospitali yoyote ni
Bure 8. Kusoma Nje ya Libya unalipiwa Kila kitu na Serikali. 9. Umeme
Bure. 10. Marufuku unywaji Pombe marufuku 11. 85% ya watu wa Libya
walikuwa wamesoma toka 25% alipochukua madaraka. 12. Hakuna Kodi Ya aina
yoyote. 13. Ukithibitika umefanya Ufisadi unanyogwa. 14. Ukiuza Bidhaa
zilizoexpiry au bandia Unanyogwa, kufungiwa leseni au faini kubwa au
vyote kwa pamoja. 15. Lita ya Mafuta Haiuzwi zaidi ya sh. 160 16. Hakuna
Riba kwenye mkopo wowote. 17. Ukinunua Gari karibia 50% unalipiwa na
Serikali na kwa wanajeshi ni 65%. Jamani Yako Mengi tu... Sasa swali
Langu ni Hili Walibya wanataka Demokrasia ili wawe kama Tanzania? maana
cc tuna demokrasia sana tu na matokeo yake ndo haya.. Walibya waliwahi
kuthubutu kusema wanatamani Maisha ya Nchi zingine sasa swali Je
wanatamani mgao wa umeme? wanatamani Ufisadi? Siwasemei moyo ila
ninachofahamu Libya ilikuwa pepo kama utaishi bila kuichokoza
serikali.... Sasa Basi cc wenye demokrasia, haki za binadamu pamoja na
utawala bora tunaishi maisha haya... Nawahakikishia Hawa Vibaraka wa
Ulaya na Marekani wanaojiita National Transition Council (NTC) kamwe
hawawezi kuipeleka Libya mahala popote zaidi ya Kuwapelekea Mafuta
mabwana Zao wazungu.., Nawakaribisha Walibya kwenye Kodi zisizo na
kichwa wala miguu,.. karibuni kwenye Lita ya mafuta 2000 kwa sababu hata
Nigeria wanachimba mafuta ila ni Gharama Kubwa kama cc.... Ningesema
mengi ila Waswahili wanasema MSIBA CHA KUJITAKIA HAUNA KILIO.. Tuombe
Uhai Tunaonana Baada Ya miaka 5 halafu tuone Libya itakuaje.... Wapi
IRAQ baada ya SADAM.., WAp AFGHANISTAN.. Iko wap KOSOVO... Kokote Nchi
za Magharibi wanapoingilia huwa hapatulii kamwe.., R.I.P Colonel"'
No comments:
Post a Comment