Friday, July 22, 2011

JANA tulichapisha habari zilizoonyesha jinsi tuhuma za rushwa zinazowakabili baadhi ya wabunge zinavyoendelea kulitikisa Bunge. Tuhuma hizo siyo tu zinaonekana kulitia doa Bunge letu tukufu, bali pia zinatishia kuzisambaratisha baadhi ya kamati za kudumu za chombo hicho cha kutunga sheria. Wahanga wa tuhuma hizo katika siku za hivi karibuni ni Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) inayoongozwa na Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema na ya Nishati na Madini iliyo chini ya Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba.
 
Mpaka sasa hakuna anayejua  lini mzimu huo wa rushwa ulianza kuzitafuna baadhi ya kamati hizo za kudumu hadi kuzifikisha hapo zilipo.  Itakumbukwa kuwa, kamati hizo zilipoundwa baada ya Bunge la Kumi kuanza kazi mwishoni mwa mwaka jana, kamati nyeti za Bunge zinazoshughulikia hesabu za Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na Mashirika ya umma zilianza kazi kwa kishindo kiasi cha kuwakuna wananchi kwa jinsi zilivyokuwa zinafanya kazi kwa ufanisi.
 
Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa, kwa mfano, ilijizolea sifa kemkemu kwa jinsi ilivyoanza kazi yake kwa mwendo wa kasi na kupambana na ufisadi katika halmashauri ilizokuwa imezikagua. Sote ni mashahidi wa jinsi kamati hiyo ilivyowashukia watendaji katika halmashauri mbalimbali nchini, kiasi cha baadhi yao kukatwa asilimia fulani ya mishahara yao baada ya  kushindwa kutoa maelehalmashauri zao.
 
Lakini kamati hiyo sasa inaelekea kusambaratika kutokana na tuhuma za rushwa zinazowakabili wajumbe wengi wa kamati hiyo, kiasi kwamba imeshindwa kukutana licha ya Mwenyekiti Mrema kuitisha vikao mara tatu kwa nyakati tofauti. Mrema mwenyewe amekiri kwamba kutokana na hali hiyo ya wajumbe wengi kutofika kwenye vikao, anakusudia kuwasilisha taarifa hiyo kwa Spika wa Bunge ili kupata mwongozo wa nini la kufanya.
 
Gazeti hili limeona taarifa rasmi za Bunge (Hansard) zinazothibitisha kuwa,  Mrema aliitisha vikao hivyo. Kitendawili ambacho sasa kimefumbuliwa ni kwamba, baada ya mjumbe wa kamati hiyo, David Kafulila kuwatuhumu bungeni wajumbe wawili wa kamati hiyo kwa kuomba rushwa kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga wakati kamati hiyo ilipokuwa inakagua miradi mbalimbali, wajumbe wengi walipata mfadhaiko na kukacha vikao ambavyo ajenda yake kuu ilikuwa kujadili tuhuma hizo za rushwa ambazo tayari zilikuwa zimemfikia Mrema na Spika mwenyewe.
 
Lakini kumbe mfadhaiko ndani ya kamati hiyo uliongezeka maradufu baada ya baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo waliokwenda mkoani Pwani kukagua miradi ya halmashauri za mkoa huo, pia kudaiwa kuomba rushwa kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiserawe ili wasiuchukulie hatua baada ya kugundua madudu katika mahesabu ya baadhi ya miradi iliyokuwa imetengewa fedha. Hiyo ndiyo siri ya kuwapo mshikemshike na mfadhaiko katika kamati hiyo na hakika, hiyo ndiyo sababu kuu inayowatia hofu wajumbe wengi wa kamati hiyo kiasi cha kuogopa kuhudhuria vikao vya kamati hiyo.
 
Kwa mwenendo huo wa wajumbe wengi wa kamati hiyo, hatuna sababu ya kutoamini kwamba halmashauri nyingine zilizokaguliwa na kamati hiyo ziliombwa rushwa lakini zilikosa ujasiri wa kutoa taarifa kwa mamlaka husika, tofauti na walivyofanya wakurugenzi wa halmashauri za wilaya za Kiserawe na Handeni.
 
Tunapoangalia uozo uliomo ndani ya kamati hiyo na kutathmini kiwango cha uozo katika Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini  na Bunge zima kwa jumla ambalo wiki iliyopita lilikumbwa na tuhuma za wabunge wake wengi kupokea rushwa ili lipitishe bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, hakika tunafadhaika na kupata mashaka juu ya mustakabali wa nchi yetu.
 
Kinachotufadhaisha zaidi ni pale Spika wa Bunge anapokaa kimya pasipo kuamuru kufanyika kwa uchunguzi huru wa Kibunge ili hatua zichukuliwe kwa wabunge waliodai au  kupokea rushwa.zo ya kuridhisha kuhusu matumizi ya fedha za Halmashauri zao

ITS TOUCHING BUT NI YA DUNIA YOTE HAYA!


UPDATE:
- Kijana amefikishwa KCMC asubuhi hii kwa msaada mkubwa wa Mhe. Hood wa Mogorogoro ambaye amejitolea kugharimia mitibabu.
- Hadi hivi sasa haijajulikana bado gharama zote za matibabu zikuwa ni kiasi gani na kama matibabu hayo yanaweza kufanyika hapa nchini au la
- Familia ya Abbas ni maskini kwa maana ya neo "maskini" na hivyo pamoja gharama hizo bado kutakuwa na mzigo mkubwa kwa familia.
- Kampuni ya Mwananchi ambao wamekuwa wakicoordinate suala hili wanafanya mpango wa kuweza kufundua Abdallah Abbas Medical Fund ya kusaidia gharama za matibabu na nyingine kwa familia. Endapo litafanikiwa hili mapema leo au siku chache zijazo itakuwa ni njia rahisi ya kuweza kuchangia kutoka sehemu yoyote duniani

Wednesday, July 20, 2011

BONGO BACK 2 UK BASH

 
COME N EXPERIENCE THE UK ENVIRONMENT IN BONGO!!;MUSIC, FOOD,DRINKS & MANY MORE....!!!

FRIDAY 22JULY@MBALAMWEZI BEACH 
ENTRY: 5:00 PM TILL LATE....ENTRY: TSH 10,000 
ITS FOR EVERYBODY WHO WOULD LIKE TO INTERACT WIT GOOD PEOPLE; EITHER YOU HAVE BEEN IN THE UK OR NOT....SHARING IDEAS OF LIFE, EDUCATION, WORK & BUSINESS..DISCUSSING THE OPPORTUNITIES EITHER IN TANZANIA OR U.K..SO ITS 4 EVERY BODY!!!!!!!   
THIS IS MORE THAN JUST A PARTY!

Tuesday, July 19, 2011

....NICOLE SCHERZINGER.....AKANUSHA NDOA....!

NICOLE SCHERZINGER - PUSSY CAT DOLLS
Msanii Nicole Scherzinger memba wa kundi la Pussycat Dolls amekanusha kuwa amechumbiwa na muendesha magari toka Uingereza,Lewis Hamilton
LEWIS HAMILTON - FORMULA 1 DRIVER
Nicole Scherzinger alitupia kwenye Twitter page kuwa yeye na Lewis Hamilton wanafunga ndoa japo amekiri kuwa wana uhusiano uliodumu kwa miaka 4 sasa,lakini hawana mpango wa kufunga ndoa kwa sasa tangu walipokuatana kwenye European Music Awards 2007,Munich-Ujerumani....
LEWIS HAMILTON vs NICOLE SCHERZINGER
Utata ulianza baada ya Baba yake Nicole kufunguka kwenye interview alipoulizwa swali kuhusu mahusiano na kufunguka kuwa “mkwe wangu mtarajiwa ni mtu poa sana,familia nzima inamkubali”

.....MTOTO MPYA WA BECKHAM....HADHARANI....!

....Ukurasa wa Facebook wa David Beckham...akitangaza kuzaliwa kwa mtoto wao wa 4....
....Baba na Mwana....!
Hatimaye familia ya Beckham imetupia kwenye mitandao mbali mbali picha za mtoto wao 'mpya' Harper Seven Beckham aliyezaliwa siku chache zilizopita pande za hospitali ya Cedars Sinai hospital,Los Angeles-Marekani...
....Victoria Beckham alipotupia kwenye tweeter..ujio wa Harper 7 Becks..!
....Mama na Mwana...!

JENNIFER LOPEZ...MARK ANTHONY....WAACHANA...!

JENNIFER LOPEZ
Artist Jennifer Lopez aka J-Lo ametangaza kuachana na mume wake ambaye ni mwanamuziki na actor,Marc Anthony baada ya miaka saba ya ndoa
MARC ANTHONY
Wote walifunguka kuwa uamuzi wa kutengana ni mgumu,na wenye kuumiza na kila mmoja anaheshimu na kukubaliana na maamuzi hayo....
JENNIFER LOPEZ vs MARK ANTHONY
J Lo na Marc Anthony walioana June 2004 pande za Beverly Hills na kwa pamoja wamezaa twins wenye miaka 3,Max na Emme waliozaliwa February 2008,Na ndoa hii ilikua ni ya 3 kwa Jennifer Lopez na ya 2 kwa Mark Anthony mwenye miaka 42 ambaye aliuza records zaidi ya milioni 11 huku Jennifer Lopez akianza muziki mwaka 1999 akitamba na hit single yake If You Had My Love

BREAKING NEWS: MBUNGE WA IGUNGA ROSTAM AZIZ AJIUZULU LEO.. WATU WAONESHA KUTOKUKUBALIANA NA KUPINGA MAAMUZI HAYO.

Mbunge wa Igunga na mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi NEC kupitia mkoa wa Tabora Rostam Aziz siku hii ya leo kwa ridhaa yake ametangaza kujiuzulu na kuachia ngazi katika nyadhifa zote alizokuwa nazo kama mjumbe wa Nec na Mbunge wa igunga,

Tamko hilo amelitoa siku hii ya leo majira ya saa tisa alasiri katika Ukumbi wa Sakao huko Igunga tabora...

Baada tu ya kutoa Tamko hilo wananchi waliokuwa eneo hilo walionekana kutoridhishwa kabisa na maamuzi hayo yaliyotolewa na kuonekana wazi kabisa wakipinga huku wakisema 'HATUTAKI" wakipinga uamuzi huo uliotolewa kwa kumtaka aendelee kuwepo kwenye nyadhifa hizo ambapo mbali na kuwa Mbunge pia alikuwa mjumbe wa NEC.


Rostam alikuwa ni mbunge wa IGUNGA kwa vipindi vinne mfululizo na alikuwa ni mjumbe wa NEC kwa Awamu tatu.

Friday, July 15, 2011

MSANII JOSE MARA ATIMIZA MIAKA 4 YA NDOA YAKE

Wazungu ndio wanaita Anniversary..
Yes Leo Mimi na Mke wangu Tumegonga Mwaka wa nne Toka Tulipofunga Ndoa.

Ni safari Ndefu isiyokuwa na kikomo, na leo ni kumbukumbu ya ndoa yetu Mke wangu upendo na uvumilivu ulionionyesha kwa kipindi hiki chote sina cha kusema zaidi ya shukrani, Mungu Atubariki sisi na Familia yetu. Nakupenda Zaidi na Nitaendelea kukupenda na kukujali Hadi Mwisho wa Maisha yangu duniani.
 
Mcheki hapa Jose Mara

Friday, July 8, 2011

the day we waited iz day we face!

KWA KILA JIPYA THEY RISE UP! BE UNTOUCHABLE FLY HIGH!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!