BREAKING NEWS: MBUNGE WA IGUNGA ROSTAM AZIZ AJIUZULU LEO.. WATU WAONESHA KUTOKUKUBALIANA NA KUPINGA MAAMUZI HAYO.

Tamko hilo amelitoa siku hii ya leo majira ya saa tisa alasiri katika Ukumbi wa Sakao huko Igunga tabora...
Baada tu ya kutoa Tamko hilo wananchi waliokuwa eneo hilo walionekana kutoridhishwa kabisa na maamuzi hayo yaliyotolewa na kuonekana wazi kabisa wakipinga huku wakisema 'HATUTAKI" wakipinga uamuzi huo uliotolewa kwa kumtaka aendelee kuwepo kwenye nyadhifa hizo ambapo mbali na kuwa Mbunge pia alikuwa mjumbe wa NEC.
Rostam alikuwa ni mbunge wa IGUNGA kwa vipindi vinne mfululizo na alikuwa ni mjumbe wa NEC kwa Awamu tatu.
No comments:
Post a Comment